CCM SONGWE YAELEZA UJIO WA MAKONDA IKIJIPANGA KWA MAPOPKEZI


CHAMA cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Songwe, chatangaza ujio wa katibu wa siasa itikadi na mafunzo Taifa Paul Makonda huku kikieleza mipango na mikakati iliyopo huku kikipongeza kazi zilizofanywa na Rais Dkt,Samia..anaripoti Ibrahim Yassin,Songwe.


Akizungumza Januari 18/2023 katibu wa siasa itikadi na uenezi (CCM) mkoani humo,Ally Yusuph amesema wanategemea kumpokea kiongozi wao Paul Makonda Februari 6/2024 akitokea mkoani Rukwa ambapo atakuwa na ziara ya siku mbili mkoani humo.


Amesema siku hiyo ya tarehe 6 atafanya kikao cha ndani cha viongozi wa chama na baadae atahutubia mkutano katika halmashauri ya mji Tunduma,kuelezea Ilani ya ccm ilivyotekelezwa na mikakati ijayo waliyoipanga.


Amesema Januari 7 atafanya mkutano wilaya ya Mbozi katika mji wa Mlowo ikiwa ni pamoja na kuzungumza na kamati ya siasa,halmashauri kuu ccm Mkoa kupitia vikao vya ndani na pia atakaa vikao vya wazee wa kimila, viongozi wa dini na wakuu wa taasisi mbalimbali.


Amesema anazungumza haya ikiwa ni jukumu lake la kikatiba ka katibu wa siasa na uenezi mkoa kueneza masuala yote ya itikadi siasa na sera za ccm akitumia Ibara ya 98 (a) ya katiba ya ccm ya mwaka 1977 toleo la Dizemba 2023.


‘Kwa mara ya kwanza Comredi Makonda ataingia kwenye mkoa wetu ,wanachama na wananchi kwa ujumla wanamsubiri kwa hamu,atazungumza mambo mbalimbali ikiwemo zikiwemo kazi zilizotukuka zilizfanywa na Rais Dr,Samia katika nchi hii hususani mkoa wa Songwe ambao umepatiwa fedha nyingi za miradi ,amesema Yusuph.


Sambamba na hilo Yusuph amesema ccm mkoa wanatarajia kufanya  ziara ya kimkakati na ya kipekee  kutembelea zaidi miradi yenye changamoto ili tujue tatizo ni nini? Kamati ya siasa itatembelea halmashauri tano za mkoa wa Songwe.


Aliitaja ratiba ya ziara kuwa ni wilaya ya Mbozi siku ya tarehe 22/01/2024, Ileje siku ya tarehe 23/01/2024,Songwe siku ya tarehe 24/01/2024,Momba siku ya tarehe 25/01/2024, na halmasha uri ya Mji Tunduma siku ya tarehe 26/01/2024.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE