CCM WAIPONGEZA TANROADS SONGWE KWA KUWAFUNGILIA FURSA WANA MOMBA

Wakala wa Ujenzi wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Songwe, unatumia zaidi ya Shilingi Million mia saba kujenga madaraja mawili katika Tarafa ya Kamsamba ili kuwasaidia wananchi katika shughuli za usafiri na usafirishaji ikiwemo wa mazao.


Kwa mujibu wa Meneja wa TANROAD Mkoa wa Songwe Mhandisi Suleiman Bishanga, Daraja la mto Nkana limegharimu fedha zaidi ya Shilingi Million miatano na limekamilika kwa asilimia mia moja.

Amesema wananchi kadhaa wameripotiwa kufariki Dunia kwenye Daraja hilo hivyo hatua ya Serikali kujenga Daraja hilo itakuwa mkombozi kwao huku Daraja lingine likigharimu zaidi ya Shilingi Million mbili.


Mhandisi Bishanga, ameiambia Kamati ya Siasa kuwa pia Serikali inajenga Daraja lingine lenye gharama ya zaidi ya Shilingi Million mia mbili lengo kubwa ikiwa ni kuhakikisha Barabara inapitika bila shida hasa ikilinganishwa na mpango wa muda mrefu wa kuunganisha Barabara katika maeneo kadhaa ya kutoka ndani ya Jimbo la Momba hadi kwenda katika maeneo ya Wilaya za Mbozi, Songwe na Chunya ikiwemo kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya kutoka Chitete hadi Utambalila Wilayani Momba kama ilivyoelekezwa kwenye Ilani ya uchaguzi.


"Hapo awali Daraja hilo lilikuwa likileta shida, katika historia kuna watu walishawahifariki kwenye daraja hili (Nkana) na daraja lilikokuwepo awali lilikuwa na mita saba tu lakini hili jipya lina mita zaidi ya ishirini", ameeleza Mhandisi Bishanga, Meneja wa TANROAD Mkoa wa Songwe.


Hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Songwe Radwell Mwampashi, angali akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa Kamati ya Siasa amewashukuru wataalam hao wa Barabara kwa namna wanavyotumia ipasavyo fedha za Umma kutekeleza miradi ya Barabara kwa manufaa ya wananchi hasa wakulima ili kusafirisha mazao yao kwa urahisi.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE