DIWANI MBOZI ATAKA SKAVETA YA HALMASHAURI IFUNGWE GPS KUDHIBITI MAPATO

 



DIWANI wa kata ya Harungu wilayani Mbozi mkoani Songwe Maarifa Mwashitete,amemshauri mwenyekiti wa halmashauri hiyo George Msyani kufunga mashine ya utambuzi (GPS) ili Skaveta waliyoinunua iweze kugundulika kazi ifanyazo..anaripoti 

Ibrahim Yassin,Songwe.

Mwashitete ameyasema hayo leo Januari 25/2024 wakati akiwakilisha hoja hiyo kwenye kikao cha baraza la madiwani cha kupitisha bajeti ya mwaka 2023/24 kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo.

Amesema halmashauri hiyo ilibuni chanzo cha mapato kununua Skaveta kwa ajili ya kuchimbia mabwawa na kutengeneza barabara ambapo kwa mtu ama kampuni kuikodi kwa siku inalipia Milioni 1 na kwamba kama hakuna usimamizi mzuri inaweza ikafanya kazi siku 6 alafu ikalipwa fedha ya siku 1.

‘’Ndugu mwandishi gari hili linakodishwa,anaweza kulikodi mtu ama kampuni akiwa nje ya wilaya kawaida kwa siku inalipiwa Milioni 1 inaweza ikakaa siku 6 badala ya kulipia Milioni 6 inalipiwa Milioni 1 hivyo ili kudhibiti mapato ni bora lifungwe Control Machine (GPS) ili liweze kusomeka linapokuwa’’anasema Mwashitete.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo George Msyani,amesema ni wazo zuri hivyo amemuagiza mkurugenzi wa halmashauri hiyo kukaa na wataalam kuona namna ya kuchakata,na kuwa walitumia Tsh,Mil,500,192 kununua gari hilo kama chanzo muhimu cha mapato.

‘’Mwaka 2022/2023 tununua skaveta hii kwa Milioni 500.192 na hadi sasa tumekusanya Milioni 79,mkakati uliopo na makisio ya mwaka tumejiwekea kukusanya Milioni 200,hoja ya diwani Mwashitete inaumuhimu na itafanyiwa kazi kuongeza tija’’anasema Msyani.

Anasema mbali na kuwa ni chanzo cha mapato pia walitumia nafasi ya kununua Skaveta hiyo kwa ajili ya kutengeneza barabara korofi ndani ya halmashauri kama kulipa fadhira kwa wananchi jamii ya wakulima ambao wanasafirisha mazao yao kwenda maeneo mbalimbali.

Katika kikao hicho amesema wamepitisha bajeti yote ya mwaka 2024/25 ambayo ni Bilioni 71.6katika matumizi mbalimbali kwenye makusanyo ya mapato ya ndani wamekadilia kukusanya Bilioni 6.3 wakati mwaka 2023/24 walikusanya Bilioni 4,6.

Akimuwakirisha mkuu wa wilaya ya Mbozi,katibu tawala wilayani humo, Mbwana Kabangwa amesema amefurahi kuona kila diwani akiinuka anazungumzia ubunifu ukusanyaji mapato,hii ni sheria namba 11 ya mwaka 2025 ya bajeti hivyo aliwataka washirikiane ili kufikia asilimi 100 ya makusanyo.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE