DIWANI MWASHITETE AISHAURI MBOZI VYANZO VIPYA VYA MAPATO YA HALMASHAURI


DIWANI wa kata kata ya Halungu katika halmashauri ya wilaya ya Mbozi mkoani Songwe,Maarifa Mwashitete (Mchumi) ameshauri halmashauri hiyo kuingiza tozo mpya za bidgaa mbalimbali ikiwemo Miwa na mazao mengine ikiwemo toza za magari stendi ili kuongeza mapato ya halmashauri...anaripoti Ibrahim Yassin,Mbozi.

Mwashitete aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati wa kikao cha baraza la madiwani cha kupitisha makadilio ya bajeti kilichoketi kwenye ukumbu wa halmashauri hiyo.

Alisema mwaka uliopita wa 2023-2024 walikusanya Bilioni 4.6 fedha ambayo ni ndogo ukilinganisha na ukubwa wa halmashauri hiyo pamoja na vyanzo vilivyopo hivyo alishauri zao la miwa linalolimwa na kusafirishwa kwenda mikoa mbalimbali nchini ushuru wake uingizwe kwenye chanzo kipya.

Alisema mwaka huu wa fedha 2024/2025 wamepitisha makadilio ya kukusanya Bilioni 6.3 na kusema ili kufikisha makusanyo hayo na hata kuvuka lengo la ukusanyaji ni lazima waainishe vyanzo vyote ikiwemo kubuni vyanzo vipya.

Diwani huyo mchumi,alivitaja vyanzo vipya vitakavyoweza kuipaisha Mbozi kimapato ni mazao kama Miwa,Magimbi,Ndizi,Pombe za kienyeji,Maparachichi na kuboresha ushuru wa machinjio na wa Magari kwenye stendi zilizopo.

‘’Ndugu mwenyekiti,magimbi na miwa inasafirishwa kiholela na hatujuhi kama kuna tozo,nashauri tozo za mazao hayo yawekwe wazi ili halmashauri ijue kiwango cha fedha kinachokusanywa hasa ushuru wa kwenye magari ambao haujatiliwa maanani’’alisema Mwashitete.

Alisema mwaka 2020/25 walibuni kujenga stendi ya magari na soko Mlowo ambapo walikuwa wakiku sanya zaidi ya Milioni 10 hadi 13 kwa mwezi na kwa siku walikusanya laki 2 hadi 4 baada ya siasa chafu kuingia magari mengi hayaingii stendi na kujikuta wakikusanya 40,000 hadi 80,000 kwa siku.

Aliongeza kuwa mwaka 2022/2023 walibuni chanzo muhimu ambapo halmashauri ilinunua gari la kuchimbia mabwawa na kulima barabara (SKAVETA) kwa Tshs,500.192 huku wakijiwekea malengo ya kukusanya Milioni 200 kwa mwaka lakini hadi sasa wamekusanya Milioni 79 pekee.

Alisema sababu kubwa ya makusanyo hayo ni udhibiti hafifu,huku akishauri gari hilo lifungwe mashine ya GPS ili kila linapokwenda kufanya kazi liwe linaonekana kwani kwa siku likikodiwa malipo yake ni Milioni 1 hivyo udhibiti na usimamizi ukiwa mzuri wanaweza kukusanya fedha nyingi.

Mwenyekiti wa halmashauri hiyo George Msyani,alisema ushauri huo ni muhimu huku akiwaagiza wakuu wa idara na watendaji vijiji na kata kuhakikisha vyanzo vyote vinaainishwa na kujulikana ili kuongeza tija ya ukusanyaji mapato.

‘’Ili kuhakikisha wapo katika makakati mzito wa ukusanyaji mapato,mnada wa Mwaswala unaofanyika mara mbili kwa wiki utahamishiwa katika stendi kuu Mlowo,wafanyabiashara wanaomwaga magimbi pembezoni mwa barabara kuu pale Mlowo waache mazao yote yaingie kwenye stendi hiyo’’alisema Msyani.

Akizungumza kwaniaba ya mkuu wa wilaya ya Mbozi,afisa tawala wa wilaya hiyo,Mbwana Kabangwa,alisema ili waweze kufikisha asilimia 100 au kuvuka lengo la ukusanyaji mapato,aliwataka madiwani na wakuu wa idara kushirikiana na kuweka mazingira mazuri ili kuvutia wawekezaji.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE