HOSPITALI YA RUFAA SONGWE YAZINDUA MASHINE YA CT SCAN,RC AIZINDUA




Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Dkt Francis  Michael, amezindua Mashine mpya ya CT Scan iliyonunuliwa na Wizara ya Afya ikigharimu fedha zaidi ya Tsh.Billion moja kwa ajili ya kusaidia kusogeza huduma za kibingwa katika Hosptiali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe iliyopo Hasamba Wilayani Mbozi.


Kwa kiwango kikubwa mashine hiyo inakwenda kutatua adha ya wagonjwa wengi kuhudumiwa/kupimwa magonjwa mbalimbali makubwa badala ya kusafiri kwenda Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na Hospitali ya Taifa Mhimbili jijini Dar es Salaam.


Akizungumza na Viongozi na baadhi ya watumishi wa Hospitali hiyo alhamisi hii (Januari 25, 2024), Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt. Francis Michael, amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia na kutoa fedha shilingi Billion 1.4 ambazo zimenunua mashine hiyo ambayo itahudumia wananchi wa ndani na nje ya nchi kutokana na Hospitali hiyo kuwa eneo ambalo ni jirani na mipaka ya nchi za SADC ikiwemo Zambia.


Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe Dr. Juma Ramadhan Juma,  amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Songwe kwa kuwazindulia mashine hiyo iliyonunuliwa na Serikali kuu ambayo itasaidia kufanya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali.


Dr. Juma, amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zaidi ya shilingi Billion moja ili kuwanusuru wana Songwe na adha ya kusafiri kwenda nje ya Mkoa kutafuta huduma za kiafya ikiwemo magonjwa ya Kansa, Kisukari na Figo.


Mkuu wa Mkoa wa Songwe aliambatana pia na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Songwe Radwell Mwampashi ambaye ameeleza kufurahishwa na namna Serikali ya Chama Cha Mapinduzi inavyoendelea kutekeleza Ilani ya uchaguzi kwa vitendo.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE