MWALIMU MBOZI ADAI KUMTEKA MTOTO NA KUMFICHA CHUMBANI AKIWA AMAFUNIKA MABLANKETI

Mwl, Baraka Mwashiuya mkazi wa kitongoji cha Tazara mamlaka ya mji mdogo wa Mlowo wilayani Mbozi mkoani Songwe,amekamatwa na jeshi la polisi pamoja na mkewe ambaye ni mwalimu wa sekondari ya Msense wakihojiwa kwa tuhuma ya kumficha mtoto wa miaka 8 chumbani…

Ibrahim Yassin,Songwe.


Akizungumza tukio hilo leo Januari 31/2024 Bibi wa mtoto huyo, Sevelina Lwesye amesema ilikuwa tarehe 29/1/2024 mjukuu wake aitwaye Bradness Kolineli Mwasote (8) hakuonekana nyumbani ndipo walipoanza kumtafuta pasipo mafanikio.


Amesema ilipofika jioni waliitaarifu serikali ya kijiji ambao waliungana nao kumtafuta na kufanikiwa pasipo mafanikio lakini walipata taarifa kwa msamalia mwema mmoja akiionesha nyumba ya mwalimu Mwashihuya ndipo walipoitaarifu jeshi la polisi waliofika na kupekuwa chumba kimoja baada ya kingine na kumkuta amefunikwa na branketi 2 pamoja na godoro.


Amesema baada ya hapo walimtoa mtoto akiwa amedhoofu kutokana na njaa ya kutokula kwa siku nzima,na kwamba baba wa mtoto huyo ni mchungaji anahuduma kanisa la TAG Mbeya ambaye amekuja na wachungaji wengine baada ya tukio kutokea.

Mchungaji Kolineli Mwasote baba wa mtoto huyo amesema alipatwa na mshangao juu ya tukio hilo huku akimshukuru mungu kwa kuwa mtoto wake amemkuta akiwa salama.


Katibu wa mwenyekiti wa kitongoji cha Tazara,Smith Muyombe licha ya kuthibitisha uwepo watukio hilo,amesema baada ya kupata taarifa hizo na kuibaini nyumba hiyo kutoka kwa msamalia mwe ma,waliitaarifu polisi ambao walikuja na kukagua chumba kimoja hadi kingine na kumkuta mtoto akifunikwa na branket 2 na godoro juu.


Muyombe amesema hilo ni tukio la pili kutokea baada ya mwishoni mwa mwaka jana alitokea mtu kuiba mtoto wa miezi minne ambaye alikamatwa na yupo gerezani na kwamba katika tukio hilo zaidi ya wananchi 71 wamejiorozesha wakitaka watuhumiwa wakitolewa wahame mtaa huo.


Kaimu kamanda wa polisi mkoani Songwe Gallus Hyera licha ya kuthibitisha uwepo wa tukio hilo ,amesema kesho atalizungumzia kwa kina kwani hadi muda leo jioni taarifa kamili haijafika mezani kwake.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE