WABUNGE NA MADIWANI WASIOWAJIBIKA WAANZA KUSHUGULIKIWA NA CCM MKOA SONGWE

Kutokana na Wadau mbalimbali kuwalalamikia Madiwani na baadhi ya Wabunge Mkoa wa Songwe kutoeleweka shughuli zao wazifanyazo katika kata na Majimbo yao Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Songwe imeanza kutoa semina elekezi kwa Madiwani pamoja na Wabunge lengo likiwa ni kuwakumbusha Majukumu yao na Wajibu wao wa kuwatumikia Wananchi na Chama pia.


Akijibu swali la wanahabari aliloulizwa Katibu wa Siasa na Hamasa Mkoa wa Songwe Yusuph Ally juu ya uwepo wa malalamiko kwa baadhi ya madiwani kulalamikiwa ni mzigo kwa Chama na wamekuwa wakijihusisha na migogoro zaidi kuliko kuwatumikia Wananchi na kutekeleza Ilani ya Chama.


Akijibu swali hilo  Yusuph Ally alikiri kuwepo kwa manunguniko hayo na Chama Mkoa kimeyasikia na tayari hatua mbalimbali zimeanza kuchukuliwa ikiwa ni pamoja kuwakumbusha Majukumu yao na kuepuka kuingilia Majukumu yasio yao


"Katibu wetu wa Mkoa tayari ameanza kuchukua hatua mbali mbali zikiwepo Semina za kuwakumbusha na kuwaelekeza Majukumu yao na kuepuka kuingia Majukumu yasio yao na kuhusu baadhi ya Wabunge kutoonekana majimboni mwao wala kufanya shughuli zozote za kimaendeleo zaidi ya kuyasifia yanayofanywa na Rais Dkt Samia hili amesema amelichukua kama Chama na atalifikisha kwa Katibu wa chama waone namna nzuri ya kufanya.


Katibu wa Siasa na siku ya Jana alifanya kikao na Waandishi wa habari kwenye lengo la mambo mbalimbali yatendwayo na CCM iliyo chini Mwenyekiti wao Dkt Samia Suluhu Hassan na amesema huo utakuwa ni utaratibu wake wa mara kwa mara

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE