RAS SONGWE ASHANGAZWA WANAFUNZI ASILIMIA 57 KUTO RIPOTI SHULE,ATOA MAAGIZO KWA UONGOZI WILAYA.
Katibu tawala mkoani Songwe Happiness Seneda ameshangazwa na kitendo cha baadhi ya wazazi kutowapeleka watoto shule kwa kisingizio cha ukosefu wa sare licha ya serikali kuruhusu watoto wavae nguo za nyumbani huku wakiendelea na utaratibu wa kushona sare.
Seneda ameyasema hayo Januari 16/2024 wakati wa ziara ya kupitia miradi ya elimu na nyumba ya mkuu wa wilaya kuona namna ujenzi ulipofikia huku akiridhishwa na hatua za ujenzi.
Akiwa katika shule mpya ya sekondari Naming’ong’o iliyojengwa kwa Milioni 583.1 Ras Seneda alishangazwa kuona shule iliyotakiwa kuchukua wanafunzi 78 wa kidato cha kwanza ni 35 pekee walioripoti huku shule mama ya sekondari Chitete iliyotakiwa wanafunzi 284 waliotipoti ni 78 pekee.
''Katika shule zote za wilaya ya Momba wanafunzi asilimia 57 hawajaripoti waliopo ni asilimia 43 pekee, natoa siku 7 kuhakikisha watoto wote wanaripoti,mzazi atakayekwamisha atachukuliwa hatua,,amesema Seneda.
Kutokana na hali hiyo amemuagiza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri na katibu tawala kusimamia zoezi zima la kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza wanaripoti hata wakiwa hawana sare.
‘’Serikali imetumia fedha nyingi kujenga shule,kitendo cha wanafunzi kutoripoti hakikubariki,Mkurugenzi,katibu tawala watendaji kata na vijiji hakikisheni mnafanya kila liwezekanalo kuhakikisha wanafunzi wote wanaripoti wazazi watakaokwamisha wachukuliwe hatua,anasema Seneda.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Momba Manoza Fabian amesema ameyapokea maagizo ya katibu tawala mkoa na kusema tatizo la Momba ni eneo la ufugaji na kilimo hivyo baadhi ya wazazi hawaoni umuhimu wa elimu hivyo wamepanga mikakati kuhakikisha wanafika shule.
‘’Tumejipanga kuhakikisha watoto wote wanatipoti shule,wazazi ama walezi watakaowatorosha watoto na kuwatumikisha mashambani au kuchunga mifugo watachukuliwa hatua za kisheria’’amesema Fabian.
Afisa elimu sekondari wilayani humo,Frorence Haule mwaka wa fedha 2022/2023 walipokea Tshs,583,180,028.00 kujenga shule Naming’ong’o kupunguza adha ya wanafunzi kutembea kilometa 26 kwenda kwenye shule mama ya Chitete na mradi upo asilimia 86.
Comments