SIASA ZA MAJI TAKA ZATAJWA KUSHUSHA MAPATO STENDI YA MLOWO KUTOKA ZAIDI YA 200,000 HADI 80,000
IMEELEZWA kuwa kutokuwepo kwa ubunifu yakinifu ya uboreshaji wa stendi kuu ya Mlowo wilayani Mbozi mkoani Songwe kumetajwa kushusha mapato yatokanayo na ushuru wa magari kutoka zaidi ya 200,000 kwa siku hadi chini ya 80,000
Ibrahim Yassin,Songwe.
Hayo yamejitokeza leo Januari 25/2024 kwenye kikao cha baraza la madiwani cha kupitisha makadilio ya bajeti kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri hiyo.
Akizungumza kwenye kikao hicho,Diwani kata ya Itaka Alani Mgula anasema mwaka 2020/25 halm
ashauri ilibuni kujenga stendi kuu Mlowo ambayo kabla hata haikukamilika ilianza kuingiza fedha nyingi kutokana na magari kuingia na kutoka lakini kwa sasa fedha inayoingia ni kidogo mno.
Naye diwani kata ya Halungu Maarifa Mwashitete anasema stendi ya Mlowo ni chanzo kikubwa ili iweze kuingiza fedha mara dufu ni bora soko la mnada wa Mwaswala uvunjwe na kuhamishiwa kwenye stendi hiyo ili kuboresha mazingira na ubora wa soko na kuingiza mapato zaidi ya halmashauri.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo,Abdallah Nandonde ,anasema ni kweli stendi hiyo ni chamzo muhimu na kilikuwa kiki ingiza zaidi ya 200,000 kwa siku lakini baada ya baadhi ya magari kutoingia kwenye stendi hiyo mapato yameshuka inafikia hadi kukusanya chini ya Tsh, 80.000
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,George Msyani,anasema ni kweli stendi hiyo ni muhimu na lilikuwa ikiingiza fedha nyingi likiini baada ya ujio wa Waziri mkuu Kassim Majaliwa wilayani humo kutaka ujenzi wa vyumba vya maduka utanuliwe magari mengi hayaingii katika soko hilo.
‘’Tunajiandaa kuwahamisha wafanyabiashara wa mazao na matunda wanaouzia kwenye soko la mnada la Mwaswala kuja kufanyia biashara zao kwenye stendi hiyo ili kuwaboreshea mazingira na halmashauri iweze kupata mapato’’anasema Msyani.
Halmashauri hiyo,imepitisha makisio ya bajeti ya Bilioni 71.6 katika matumizi mbalimbali huku maku sanyo ya mapato ya ndani wamekadilia kukusanya Bilioni 6.3 badala ya Bilioni 4.6 waliyokusanya mwaka jana,
Comments