TANESCO YAWAHITAJI WAKANDARASI WA KIKE
DAR ES SALAAM: KUTOKANA na uwepo wa ushiriki mdogo wa wahindisi wakike katika Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), shirika hilo limezindua mpango wa uwezeshaji wa wahandisi wakike( WECDP) kama sehemu ya kuhamisisha masuala ya kijinsia kushiriki katika shughuli za uendelezaji wa miradi ya umeme nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo uliofanyika leo Januari 29,2024, jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga amesema kutokana na kuwepo kwa idadi ndogo ya wahandisi wanawake shirika hilo limeamua kuanzisha mkakati maalumu utakao saidia kuwepo kwa wahandisi wengi wakike watakaoajiriwa na kufanya kazi na shirika.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Seif Shekilagha ameahidi kuwa wizara itaendelea kutoa ushirikiano kwa shirika hilo na kuufanya mradi huo kuwa mfano.
Aidha, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof Nelson Boniface aliyemwakilisha makamu wa chuo hicho amesema kuwa kutokana na programu hiyo wanatarajia kuwawezesha wanawake katika tafiti ili waweze kusaidia kutatua changamoto maalumu zinazolikabilu shirika hilo.
Mmoja wa wanufaika wa mradi huo Mhandisi Catherini Mwigohi, amesema mradi huo utawasaidia kupata uzoefu na ujuzi utakao saidia kuongeza uzalishaji na uwezo katika uongozi ndani ya shirika hilo.
Mradi huo umeanzishwa kupitia mradi wa Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia na Shirika la Misaada la Ufaransa na unatarajiwa kudumu kwa miaka minne kuanzia mwaka 2023 hadi mwaka 2026, huku ukitegemewa kuongeza 7% za wanawake katika nafasi mbalimbali za kufanya maamzi na kuwajengea uwezo wahandisi wanawake waweze kuajirika ndani na nje ya shirika hilo
Comments