KIHENZILE:AITAKA TAA KUVUNJA MKATABA NA MKANDARASI



 Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile ameelekeza mamlaka wa viwanja  vya ndege Tanzania (TAA) kuvunja mkataba na Mkandarasi anayejenga jengo la abiria la kiwanja cha ndege cha Ruvuma kutoka na Mkandarasi huyo kushindwa kukamilisha jengo hilo kwa wakati.

Kihenzile ameyasema hayo baada ya kutembelea na kukagua maboresho makubwa yaliyofanywa katika uwanja wa Ndege wa Songea.

“Serikali imewekeza bilioni 37  katika  uwanja wa ndege  huu, hivyo ni muhimu jengo la abiria likamilike kwa haraka. Nauelekeza uongozi wa TAA kuvunja mkataba  na Mkandarasi anayejenga Jengo la Abiria kwani ameshindwa kukamisha kwa wakati ,Alisema Kihenzile

Jengo hilo la abiria lilitakiwa kukamika mwezi wa sita mwaka jana lakini mkapa sasa lipo asilimia 30 na Ujenzi wake unathamani ya shilingi milioni mianne ishilini na tatu (423) lakini ujenzi   umesimama kutokana na  changamoto za mkandarasi

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Songea  Kapenjama Ndile amesema kuwa uwanja wa Ndege wa Songea ni muhimu kwa  usafishaji wa Mizigo na Abiria kutoka  nchi jirani kama vile Msumbiji na Malawi pia usafirishaji wa mazao ya Mboga mboga na matunda kama vile parachichi  hivyo wananchi wa Songea na Mikoa jirani ni Muhimu kutumia uwanja huu ,alisema  Ndile

Awali  Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Songea   Mhandisi  Danstan Komba akisoma taarifa ya uwanja wa ndege huo amesema kuwa ujenzi wa Barabara ya ndege (Run way) umekamilika ,ujenzi wa barabara ya kiungio (Taxing Way) umekalika,Ujenzi wa kiuto cha nishati umekalika  hivyo bado jengo la abiria .

Uwanja wa ndege wa Songea ni mojawapo ya viwanja vya ndege vilivyojengwa kuanzia mwaka 1974  kikiwa na barabara ya kutu ana kuruka ndege kwa kiwango cha changarawe, lakini sasa serikali umeboresha uwanja huo na wakuwa uwanja wa kisasa.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE