MAJALIWA AMUWEKA NDANI MAHASIBU KWA UPOTEVU WA MILIONI 213
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, ACP Salum Morcase kumkamata Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Saad Matunzi kwa kosa la kuhamisha fedha Sh milioni 213.748 kwa matumizi binafsi.
Majaliwa ametoa agizo hilo leo jioni alipozungumza na madiwani na watumishi wa halmashauri hiyo mkoani Mara.
Imeelezwa kuwa fedha hizo zilihamishwa kwa awamu nne, kwa njia ya uhamisho wa ndani, ambapo mhasibu huyo alishirikiana watumisi wa Ofisi ya Rais Tamisemi.
Mkamate huyo bwana sasa hivi aende polisi akafunguliwe mashtaka, huyu ni wakupeleka mahakamani moja kwa moja, DPP aelezwe afungue jalada la mashtaka, wale wenzake tumewapeleka mahakamani tayari, kwasababu tulibaini walihusika na wizi kama huu kwenye Manispaa ya Kigoma mwaka jana”. amesema Waziri Mkuu.
Comments