TANROAD WAAGIZWA KUMUONDOA MKANDARASI


 MOROGORO: Wakala wa Barabara (TANROADS) ameagizwa kumuondoa Mkandarasi wa Kampuni ya Kay Bouvet Engineering Ltd ya Nchini India na kumtafuta Mkandarasi mwingine mwenye uwezo na sifa za kujenga miundombinu ya barabara katika Kiwanda cha Sukari cha Mkulazi


Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa aliyedai kutoridhishwa na utendaji wa Mkandarasi huyo. Amesema “Mkandarasi huyu ni mbabaishaji na tumeamua kumuondoa kwa kuwa hana mitambo ya kutosha ya kutekeleza kazi ya ujenzi wa barabara, pia hana sifa na uzoefu wa barabara kwa kiwango cha lami.”


Baada ya hatua hiyo, Bashungwa ameuagiza Mtendaji Mkuu wa TANROADS kutangaza zabuni ya mradi huo huku akisisitiza kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya kiwanda hicho alichosema kimechofikia 70% na kuwa kitasaidia kuongeza uzalishaji wa Sukari Nchini


Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE