DAWATI LA JINSIA MOMBA WATETA NA WANAFUNZI TUNDUMA


Mkuu wa kitengo cha Dawati la Jinsia na Watoto Wilaya ya Momba Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Bahati Simchile amewataka wanafunzi wa Shule ya Sekondari Danida iliyopo Mjini Tunduma Mkoani Songwe kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto kwa Jeshi la Polisi pindi wafanyiwapo au waonapo ili aweze kuzichukulia hatua za haraka.

Alisema hayo Machi 26, 2024 alipotembelea Shule hiyo kwaajili ya kutoa Elimu ya masuala ya Ukatili wa kijinsia ambapo amewafundisha nini maana ya ukatili, sababu, aina, madhara ya ukatili na jinsi ya kuepuka kufanyiwa vitendo hivyo pindi wawapo shuleni, njiani, nyumbani na mtaani.


Kwa upande wa wanafunzi hao wameahidi awatokaa kimya watatoa taarifa za ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto kwa Jeshi la Polisi ili kupunguza vitendo hivyo katika jamii.


Kutoka Dawati la Habari Polisi Songwe.






Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE