DEREVA WA GARI LA SERIKALI MIKONO MWA POLISI KWA KUMJERUHI MWANAE

 JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia Dereva wa serikali, James Mrema kwa tuhuma za kumfanyia ukatili kwa kumpiga na kumsababishia maumivu makali mtoto wake mwenye umri wa miaka tisa.


Akizungumza na Nipashe Digital kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Theopista Mallya, amesema "Jeshi la polisi linamshikilia dereva wa gari la serikali aliyefahamika kwa jina James Mrema(39) kwa kumpiga mtoto wake na kumsababishia maumivu makali hadi kulazwa katika hospitali ya rufani ya Mkoa wa Dodoma."

Amesema jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi juu ya tukio hilo na utakapo kamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.Awali, Dk.Baraka Monday wa Hospitali ya Rufani ya mkoa wa Dodoma, amekiri kupokelewa kwa mtoto huyo hospitalini hapo na mwili wake umekutwa na majeraha ya kupigwa huku mguu na mkono ukiwa umevimba.


Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE