HII HAPA MIRADI MIKUBWA TISA YA KIMKAKATI MKOANI SONGWE INAYOTEKELEZWA NA TANROADS

 


Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imekusudia kutekeleza miradi mikubwa 9 ya kimkakati 9 ikiwemo upanuzi wa barabara kuu ya TANZAM kipande cha Igawa – Tunduma (km 218) na Ujenzi wa kituo cha ukaguzi wa pamoja wa magari katika barabara hiyo eneo la Iboya Mkoani Songwe.

Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Songwe Mha. Suleiman Bishanga amesema hayo tarehe 19 Machi 2024; alipozungumza na Kipindi cha TANROADS Mkoa kwa Mkoa kuhusu mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita katika sekta ya ujenzi wa miundombinu ya barabara na madaraja.

Amemtaja mkandarasi anayejenga barabara hiyo ya njia nne kwa utaratibu wa EPC + F ni M/s China Civil and Engineering Construction Coopration (CCECC) kutoka China; ambaye tayari ameshaanza maandalizi ya kuainisha maeneo ya kujenga kambi.


Amesema pia mradi huo utakuwa na barabara za mchepuo (Bypass) ili kuondoa msongamano wa magari hasa malori katikati ya mji.

Amesema miradi mingine ambayo ipo kwenye mipango ya Serikali katika ujenzi ni Barabara ya Mlowo – Kamsamba na Spur Road ya Chitete Makao Makuu ya Wilaya ya Momba (Km 147) na tayari imeshakamilisha ujenzi wa daraja la Momba linalounganisha Mkoa wa Songwe na Rukwa.

Pia Barabara ya Isongole II – Ngana / Mbeya – Kasumulu hadi Katumbosongwe Km 124). Sehemu ya Kwanza ya Isongole II – Ibungu – Isoko (Km 52.419) ujenzi unatarajia kuanza hivi karibuni kwani zabuni ilishatangazwa na kumpata mkandarasi wa kujenga kwa kiwango cha lami barabara hiyo na ulipaji wa fidia wa mali, nyumba na mazao umeshakamilika ambapo waathiriwa wa mradi wapatao 312 wamelipwa fidia ya jumla ya TZS Milioni 850.269


Barabara ya Ruanda – Nyimbili – Izilya – Itumba (Km 79) na Mahenje – Haasamba – Vwawa Km 32. Sehemu ya kwanza km 1.2 Mkandarasi aitwae GNMS Contractors C. Ltd kutoka Iringa anaendelea na kazi; sehemu iliyobaki ya Ruanda – Idiwili km 20 imetengwa sehemu nne za km 5 kila moja ambapo ujenzi wa kiwango cha lami wa sehemu hiyo utafanywa na Wakandarasi Wanawake.


Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE