MBUNGE SENDEKA ANUSULIKA KUUWAWA KWA RISASI NA DEREVA WAKE



 ARUSHA: Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole- Sendeka (CCM) amesema yeye na dereva wake hawakuumia katika jaribio la kuuawa baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana wakati akielekea jimboni kwake.


“Ni kweli tumeshambuliwa na watu ambao haikuwa rahisi kuwafahamu kwa wakati ule. Walikuwa kwenye gari wakitufuata na tulipofika kati ya kijiji cha Ng’abolo na Ndido katika wilaya ya Kiteto walianza kutushambulia,” amesema Ole Sendeka. “Ni kama risasi nne au tano hivi tulizoona kwa sasa … nilianza kufyatua risasi muda ule walivyoanza kutufyatulia risasi na kwa bahati dereva alibadili mwelekeo na ndio pona yetu.”

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Lucas Mwakatundu amethibitisha kuwa tukio hilo limetokea jioni ya leo Ijumaa Machi 29, 2024, majira ya saa 12:45 jioni.

Amesema polisi inaendelea na uchunguzi, hata hivyo Ole Sendeka na dereva wake wote ni wazima na hawakudhurika kabisa.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE