RPC MALLYA AKABIDHIWA OFISI DODOMA
Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Theopista Mallya Machi 20, 2024 amekabidhiwa rasmi Ofisi kama Kamanda wa mkoa huo baada ya kuhamishwa kutoka mkoa wa Songwe.
Wakati wa makabidhiano hayo, Kamanda Mallya alimshukuru aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa huo SACP Martine Otieno baada ya kumkabidhi Ofisi hiyo na kuhaidi kuendelea kudumisha amani ya mkoa wa Dodoma.
Pia, Kamanda Mallya aliwataka Polisi Kata kuendelea kutoa elimu ya Polisi jamii kwa kukemea uhalifu kwa kuanza na ulinzi shirikishi na kuhakikisha kila kata inakomesha uhalifu kikamilifu. Lakini pia amewataka Wakuu wa Polisi Wilaya (OCD's) kusimamia kata zao ili kuweza kuondoa uhalifu na kuifanya Dodoma kuwa salama.
Comments