SIKUKUU INAPITA, UHAI AUNUNULIWI



Madereva na wamiliki wa vyombo vya moto mkoani Songwe wametakiwa kuendelea kufuata sheria za usalama barabarani ili kujiepusha na ajali zinazoweza kuepukika kuelekea kipindi cha sikukuu ya Pasaka.


Rai hiyo imetolewa na Polisi Kata ya Ipunga Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Eletisia Mtweve Machi 26, 2024 wakati alipokua anatoa elimu juu ya thamani ya uhai wa mwanadamu kwa waendesha pikipiki za magurudumu mawili maarufu Bodaboda katika Kijiwe cha Shingo Fene kilichopo Kijiji cha Ipunga wilayani Mbozi.



“Kumbukeni uhai aununuliwi sehemu yoyote hapa duniani hivyo ni wajibu wenu kufuata sheria za usalama barabarani ikiwa ni pamoja na kujiepusha na matumizi ya dawa za kulevya, pombe na kujiepusha kubeba abiria usiyemfahamu nyakati za usiku ukiwa peke yako ili kulinda usalama wako kwanza" alisema Mkaguzi Mtweve.


Aidha, alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wazazi/walezi na jamii kiujumla kuendelea kuwa karibu na watoto wao katika nyakati hizi za mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo ili kuwaepusha na madhara yanayoweza kusababishwa na mvua hizo ikiwemo kifo.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE