TUCHUKUE TAHADHARI KUELEKEA KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU YA PASAKA

Wananchi wa Mkoa wa Songwe wametakiwa kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya Pasaka.


Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Agustino Senga wakati akizungumza kupitia kipindi maalum cha redio Tunduma Fm 92.1 MHz"iliyopo mjini Tunduma Machi 28, 2024.


Kamanda Senga aliwataka wananchi kuchukua tahadhari

mbalimbali hasa katika kipindi hiki cha kuelekea kipindi cha

sikukuu ya Pasaka kutokana na mvua zinazonyesha akiwataka kuepuka

kukaa mabondeni na kuwakataza watoto kucheza na

kuogelea kwenye madibwi na mito hasa ukizingatia kwa sasa watoto wengi wapo mikononi mwa wazazi kutokana na kufungwa

kwa Shule.


Aidha, Kamanda Senga aliwasihi wananchi kuepukana na unywaji wa pombe uliopindukia  ambao unaweza kupelekea wafanye vitendo vya kihalifu na ukatili katika jamii na kufanya hivyo Jeshi la Polisi litachukua hatua kali kwa watu hao.


Pia Kamanda Senga aliwataka madereva kufuata sheria za usalama barabarani na

kuachana na tabia ya kuendesha gari kwa mwendokasi ikiwa

ni pamoja na kuyapita magari mengine sehemu zisizoruhusiwa.


Kamanda Senga aliomba ushirikiano kutoka kwa jamii katika ulinzi wa watoto katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya Pasaka kwani watoto wengi watakuwa maeneo mbalimbali kusherekea sikukuu hiyo hivyo kila mwananchi anapaswa kulinda usalama wa mtoto pale anapoona akifanyiwa ukatili au anapocheza michezo ambayo inaweza kuhatarisha maisha yake ili watoto wawe salama katika kipindi hicho cha sikukuu.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limejipanga vema katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya Pasaka kwa kuendelea kuimarisha ulinzi kuanzia ngazi ya Kata kwa kutumia vikundi vya ulinzi shirikishi vikiongozwa na Polisi kata wa eneo husika ikiwa ni pamoja na askari kuendelea kufanya doria maeneo yote ya mkoa katika kuhakikisha usalama wa raia na mali zao.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE