UJENZI WA DARAJA LENYE KIVUKO CHA CHINI (UNDERPASS) MBOZI LAKAMILIKA ASILIMIA 65
Hayo yamebainishwa na Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Songwe Mhandisi Suleiman Bishanga huku akisema kuwa mradi huo ni moja kati ya miradi inayotekelezwa Mkoani Songwe ambao utaenda kubadilisha Mji wa Ruanda na kufungua fursa mbalimbali kWa wakazi na watumiaji wa barabara hiyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi na watumiaji wa barabara ya Ruanda Isongole kupitia iyula ambako mradi huo unajengwa wameishukuru Serikali chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa daraja hilo huku wakiomba likamilike kwa wakati ili fursa wazipate ikiwemo ya urahisi wa usafirishaji wa mazao yao kupitia barabara hiyo.
Comments