WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA JESHI LA POLISI ILI KUTOKOMEZA UKATILI


Wazazi na walezi wilayani Mbozi wametakiwa kuendelea kushirikana kwa ukaribu na Jeshi la Polisi ili kuweza kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vinavyojitokeza kwenye jamii.


Akizungumza wakati alipohudhuria Ibada ya misa takatifu ya Sikukuu ya Pasaka katika kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Mbeya Parokia ya

Mtakatifu Patrick, Machi 31, 2024, Kamanda wa Polisi mkoani Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Agustino Senga, alisema ni vyema wazazi na walezi kukaa karibu na watoto wao ili kujua ukatili wanaofanyiwa ili kubaini na kudhibiti ukatili huo mapema kwa kutoa taarifa Polisi kwani kufanya hivyo kutapunguza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.

Aidha, Kamanda Senga alisema ili kuwa na kizazi bora na chenye maadili na kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji dhidi ya watoto ni lazima kuimarisha malezi bora kwa watoto kwa kuwapa nafasi ya kuwasikiliza na kuwa karibu nao ikiwa ni pamoja na kufuatilia mabadiliko ya tabia zao.

 “Haya maovu yanayotokea katika jamii yetu, sisi waumini tuna nafasi kubwa ya kupambana na matendo yote maovu katika jamii hasa sisi tunaokuja kwenye nyumba za ibada ukisali na ukimjua Mungu lazima utakuwa mtu mwema sana basi tuendapo huko majumbani tuyatende yale yanayompendeza Mungu ili jamii iige kwani Songwe bila ulawiti, ubakaji na uhalifu inawezekana” alisema Kamanda Senga.

Utoaji huo wa elimu kwenye nyumba za ibada ni sehemu ya kupinga vitendo vya ukatili ambavyo vinaleta madhara makubwa katika jamii.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE