ACHENI TABIA ZA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI


 Wananchi wa Kijiji cha Itewe Kata ya Itaka Wilaya ya Mbozi Mkoani Songwe wametakiwa kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi pindi uhalifu unapotokea katika maeneo yao bali wametakiwa kutoa taarifa hizo kwa Jeshi la Polisi ili ziweze kushughulikiwa kwa haraka.


Rai hiyo ilitolewa na Mkuu wa Upelelezi na Makosa ya Jinai Wilaya ya Mbozi Mrakibu Msaidizi wa Polisi ASP Julias Kishai Aprili 23, 2024 alipofika kijijini hapo kutoa elimu juu ya madhara ya kujichukulia sheria mkononi.


Mrakibu Kishai alisema “acheni kujichukulia sheria mkononi toeni taarifa za uhalifu na wahalifu, katika kituo cha Polisi kilichopo karibu nanyi ikiwa ni pamoja na kuwakamata wahalifu hao na kuwafikisha kituo cha Polisi au kwa viongozi wa amani ili taratibu za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Naye Polisi Kata wa Kata hiyo Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Kajembula Mwakalinga aliwataka wananchi wa kijiji hicho kuacha tabia ya kuziamini imani za kishilikina ambazo zinapelekea mtu kujichukulia sheria mkononi bila kufuata taratibu za kisheria ili kuepusha madhara katika jamii.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE