CHONGOLO KUANZA ILEJE KESHO



Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo anatarajia kuanza ziara ya kikazi Wilayani Ileje kuanzia tarehe 28-01 Mei ikiwa ni ziara yake ya kwanza wilayani tangu aliteuliwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Songwe.Katika ziara hiyo Chongolo anatarajia kuambata na timu ya wataalamu toka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe wakiongozwa na Katibu tawala wa Mkoa wa Songwe Happiness Seneda.

Kwa mujibu wa ratiba iliotolewa na Halmashauri ya Ileje Chongolo atapokelewa Mbebe saa tano asubuhi Kisha kuelekea shule ya wasichana Ileje sekondari katika ziara hiyo Chongolo atakuwa na mkutano wa hadhara na Wananchi uwanja wa Itumba na pia atakutana na Madiwani na Kamati ya Siasa kabla ya kukutana na watumishi wa Ileje.


Kabla ya kurejea Mkoa Songwe Chongolo anatarajia kufanya Mikutano mitatu ya hadhara kata tofauti na pia anatarajia kuwa mgeni rasmi siku ya Wafanyakazi Mei mosi.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE