MIMBA ZA UTOTO ILEJE ZAMCHEFUA CHONGOLO AWEKA MIKAKATI MIZITO NA POLISI

Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Daniel Chongolo amekemea vikali tabia ya uwepo wa mimba za utotoni hususani wanafunzi katika Wilaya ya Ileje ambapo amesema katika utawala wake hakuna mtu yeyote atakayekwepa mkono wa dola kwa kumpatia mimba mwanafunzi.


RC Chongolo ameyasema hayo leo Aprili 28 wakati akiongea na wananchi katika ziara yake eneo la Shule ya Sekondari ya Wasichana (Ileje Girls) iliyopo kijiji cha Ikumbilo Kata ya Chitete wilayani Ileje.

"Niwaambie wala hatutaki kusema mengi ambao wao hawawezi kuacha mabinti wadogo wasome, tutawasaidia kwenda kufanya kazi nyingine zitakazofaa zaidi ili wasionane na mabinti kwa miaka 10,20,25 mpaka 30 ili wakirudi watakuwa walimu wazuri." amesema RC Chongolo


Mhe. Chongolo anatarajiwa kuendelea na ziara yake kesho kukagua miradi mbalimbali ikiwa ni sehemu ya mwendelezo wa ziara yake ya kikazi ya siku 3 ndani ya wilaya hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE