DC KIHONGOSI ATAJA BIL,124 ZIMETUMIKA UJENZI WA MIRADI MOMBA



Mkuu wa wilaya ya Momba mkoani Songwe Kennan Kihongosi ame tumia sherehe za  siku ya Muungano wa Tanganyika kutaja mafanikio ya miaka mitatu ya Rais Dkt,Samia Suluhu akisema alitoa Bilioni 124 zilizojenga miradi....anaripoti Ibrahim Yassin,Songwe.


Alisema serikali ya awamu ya sita inafanya kazi kubwa ya kuwa ondolea wananchi changamoto zinazowakumba hivyo kazi iliyopo ni kuhakikisha miradi inatunza ili iweze kusaidia hadi vizazi vijavyo kwa ni amegusa kila sekta ikiwemo Elimu, ,Afya ,Maji, Miundo mbinu na Nishati.


Dc Kihongosi aliyasema hayo jana Aprili 26/2024 wakati wa maadhi misho ya miaka 60 ya uhuru wa Tanzania na Zanzibar yaliyofanyika kijiji na kata ya Kamsamba wilayani Momba mkoani humo.


Alisema kwenye elimu zimetumika,Bilioni 31,Afya Bilioni 14.4,Vifaa Tiba Bilioni 1.6 Maji Bilioni 17.8 huku vitongoji 142 vikiwekewa ume me ambapo vitongoji 153 kazi inaendelea na pia Bilioni 6 zikitumika ujenzi wa barabara,makalavati na madaraja ndani ya miaka mitatu.

Alisema katika kipindi cha mwaka 2021 hadi 2024 cha utawala wa ke wa mika 3 Rais Dkt,wilaya ya Momba ilipokea Tsh,124,062 ,121,57 4.23 ikiwa ni kiasi cha Tsh,45,499,583,419.41 zilienda halma shaurin ya mji Tunduma na Tsh,31,870,007,687.56 zilienda halmashauri ya Momba.


Aliongeza kuwa katika sekta ya kilimo mifugo,wameweza kujenga miradi ya kimkakati, Soko la kimataifa la mazao na mifugo kakozi,(Ma ghara ya kuhifadhia mazao),jengo la kuuzia mazao,mnada wa mifugo na jengo la machinjio na pia pikipiki 23 zilinunuliwa kwa ajili ya maafi sa kilimo zikiwemo 8 zilizonunuliwa kwa fedha za mapato ya ndani.

Aliongeza kuwa ujenzi wa majosho 6 ya kuogeshea mifugo imeje ngwa kwenye vijiji vya Chitete,Msangano,Nzoka,Ivuna,Mkulwe na Mkomba huku ununuzi na usambazaji wa mbegu za ufuta kwa waku lima ukifanyika kuwaongezea tija na hamasa ya stakabadhi ghala ni,ikiwemo ununuzi wa chanjo za mifugo.


Alieleza kuwa Kiasi cha Tsh,1,974,892,771.14 kilitumika kwa ajili ya sensa ya watu na makazi ya 2022 ambapo wilaya ya Momba yenye wakazi 551,090 na kaya 114,687 ambapo halmashauri ya Momba yenye wakazi 259,781 na kaya 58,098 na halmashauri ya Tunduma ina wakazi 291309 na kaya 56,589.


‘’Leo ni kilele cha Muungano ambapo waasisi wa nchi hii mahayati Mwali Julias Nyerere na Abed Kalume mwaka 1964 walikubaliana Zanzibar na Tanganyika kuuungana,hivyo kuna kila sababu ya kuui marisha na kuulinda muungano huo,na tayari tumeona maendeleo mengi yakifanyika.


Nae shekhe mkuu mkoani humo,Husein Batuza alisema wao kama viongozi wa dini wana kila sababu ya kuliombea Taifa na viongozi wa ke huku a kimsifu Rais Dkt,Samia kwa kupeleka fedha nyingi mkoani Songwe zilizojenga miradi ya maendeleo inayogusa jamii.


Diwani mwenyeji Chalambwenge Kakwale,katika maadhimisho hayo mbali na kuipongeza serikali kupeleka fedha nyingi za miradi iliyojengwa hata kwenye kata yake,lakini alitumia nafasi hiyo kutoa kero za ukosefu wa Xray Mashine kwenye kituo cha afya Kamsamba ambapo mkuu wa wilaya ameahidi kuifanyia kazi.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE