TANROADS SONGWE WAPAMBANA USIKU NA MCHANA KUREJESHA MAWASILIANO BARABARA YA SHIGAMBA NA IBABA ILEJE


 Kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha wilayani ileje na kusababisha utelezi, mmomonyoko (landslide) Kupelekea magari kukwama kwa muda katika barabara ya Shigamba kwenda Ibaba hivyo kuwa kero kwa abiria na mizig. Serikali kupitia wizara ya ujenzi na Wakala ya Barabara Mkoa wa songwe wamefanya jitihada za haraka na kunasua magari yote na tayari vifaa vya kurejesha mawasiliano vinaendela kumalizia zoezi la kuireja mawasiliano

Aidha, kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Meneja wa Mkoa Tanroads mkoa wa Songwe Mhandisi Suleiman Bishanga amemtaka mkandarasi kuongeza magari kwa ajili ya kusomba kifusi ambacho kinahimili hali ya mvua na pia kufanya kazi usiku na mchana ili kukabiliana na hali ya mvua zinazoendelea

Meneja amemshukuru Mhe.Dkt Samia S. Hassan  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha za dharura ambazo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kuwezesha kuondoa changamoto za matengenezo ya barabara. 


Sambamba na hilo amemshuku Mhe Innocent Bashungwa Waziri wa Ujenzi na Mtendaji Mkuu wa Tanroads Mha. Mohammed Besta kwa ushirikiano na mwongozo wakati wa utatuzi wa changamoto.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE