MWALIMU ATOKA NDUKI SHULENI KUWAKIMBIA WANAOMDAI

 


WANAFUNZI wa Shule ya Msingi Luwa katika Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa, walikatisha masomo kwa takribani saa tatu baada ya wajasiliamali kufika shuleni hapo na kumfanyia shambulio la aibu Mwalimu Mkuu wa Shule kwa madai ya kushinikiza walipwe fedha wanazomdai mwalimu aliyekopa bidhaa kwao.


Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Mwenyekiti wa Kijiji, Stedius Pastory, amesema tukio hilo lilitokea majira ya saa 3 asubuhi wakati mwalimu waliyekuwa wakimdai akiwa shuleni hapo akiendelea na majukumu yake.

Amesema mwalimu aliyedaiwa baada ya kuwaona wajasiriamali hao wakifika shuleni hapo na gari lao, ghafla alitimua mbio na kukimbilia kwenye shamba la mahindi karibu na shule hiyo ndipo mmoja kati yao alianza kumkimbiza.

“Baada ya kushindwa kumkamata, alirejea katika eneo la shule na kuungana na mwenzake aliyekuwa amebaki kwenye gari na kwenda moja kwa moja walimvamia ia mwalimu mkuu aliyekuwa akizungumza na wazazi wa wanafunzi waliokuwa wamefika kulipa michango kisha kumkaba, kumkatia vishikizo vya shati na kupasua simu janja yake.

Wakati wajasiliamali hao wakifanya vitendo hivyo, wazazi waliokuwapo eneo hilo waliwakamata na kuwazuia wajasiliamali hao ndipo mwalimu mkuu alipokimbilia ofisini kwake na kujifungia ili kujinusuru na hasira za watu hao.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE