NCHIMBI APIGA MARUFUKU KUENDELEZA MAKUNDI BAADA YA UCHAGUZI WA NDANI

"Niwasihi wana CCM kataeni viongozi wa kuandikiwa, wa kuletwa mfukoni ninyi mnaishi na watu kwenye maeneo yenu na mnawajua , chagueni watu kwa sifa na mtu apewe kwa sifa zake sio za rafiki au mpambe wake"


"...lakini tujue kwenye uchaguzi kuna kusinda na kushindwa hivyo ni lazima tukubali matokeo mara baada ya chaguzi"



"Makosa makubwa ni kuendeleza makundi ya uchaguzi baada ya uchaguzi , makundi yaishe mara tu baada ya uchaguzi kutangazwa"

"Nafasi kubwa kulikonzote ndani ya CCM ni UANACHAMA, usichaguliwe kuwa kiongozi ukajiona wewe ndio mkubwa kuliko wote, wewe ni mtumishi na mda wowote unaweza kutumika sehemu nyingine kwa maslahi ya watu wote na sio kutumia nafasi yak kwa kuweka makundi"


"Viongozi lazima watambue nafasi zao za utumishi, ukiwa Mbunge unajua wewe ni mtumishi wa wananchi wako, ukiwa Waziri utambue wewe ni mtumisi wa wananchi wako ukitaka kujifanya boss lazima utapata changamoto kwenye uendeshaji wa eneo lako"

Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi
Katibu Mkuu wa CCM

Akizungumza na Mabalozi wa mashina, Viongozi mbalimbali wa serikali, Taasisi zisizo za kiserikali, Wazee na Viongozi wa Dini.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE