RC CHONGOLO APONGEZA UKUSANYAJI MAPATO TRA ILEJE AKIPOKEA CHANGAMOTO.
Serikali imeombwa kukipandisha hadhi kituo cha forodha cha Isongole wilayani Ileje Mkoani Songwe kutoka daraja C kwenda B pamoja na ujenzi wa majengo yenye hadhi mpakani....anaripoti Ibrahim Yassin,Songwe
Leo Aprili 28/2024 Afisa mfawidhi kituo cha forodha Isongole katika mpaka wa Tanzania na Malawi Charles Chacha.baada ya mkuu wa Mkoa huo Daniel Chongolo kukaguana kupokea taarifa ya shughuli zinazotekelezwa mpakani hapo.
Chacha amesema kutokana na kituo hicho kutokuwa na hadhi ,kwa sasa kinafanya kazi kama pacha na kituo cha forodha chaTunduma mpakani mwa Tanzania na Zambia
Chacha amesema serikali inatakiwa kukipandisha hadhi kituo hicho kimekidhi vigezo vya kuongeza wigo wa ukusabyaji mapato kutoka Sh 7.8 milioni mwaka 2019 mpaka kufikia zaidi ya Sh 400 mwaka 2024 licha ya mpaka huo kuwa na vipenyo vinavyopelekea mapato mengi kupotea.
Amesema mpaka huo unapitisha bidhaa mbalimbali zinazoingia na kutoka ikiwepo, zao la Mahindi, Soya, Karanga, vinywaji, saruji ambavyo husaidia mapato kuongezwa hivyo kuna haja kupandishwa hadhi kwa mpaka huo.
Chacha amesema kituo hicho kinatakiwa kijengwe majengo yenye hadhi ya mpaka kwani yaliyopo hayaendani na hadhi ya mpaka ambapo kituo hicho kinafanya kazi kwa karibu na kituo cha forodha cha Tunduma ambacho mpaka wa Tanzania na Zambia.
"Kituo hiki kina uhaba mkubwa wa watumishi kwenye idara ya Tbs, Takukuru, wakala wa misitu Tanzania(TFS), na kushauri idara ya kilimo iwezeshwe kifaa cha kupima ubora wa mazao yanaoingia nchini kuputia mpaka huo," amesema Chacha
Kwa upande wake mkuu wa mkoa huo Daniel Chongolo amesema atahakikisha analifikisha ombi hilo kwenye mamlaka zinazohusika ili kufanikisha upandishw aji hadhi wa kituo hicho ambacho ni lango la biashara na fursa za kiuchumi kwa wananchi.
Chongolo amesema wakati serikali ikijipanga kupandisha hadhi kutua hicho kutoka daraja C kwenda daraja B viongozi waliopewa jukumu la kusimamia mpaka huo wahakikishe wanadhibiti uvushaji bidhaa kwa njia ya magendo na mbolea za Ruzuku.
Comments