SONGWE YATAJA MAFANIKO YA SEKTA YA ELIMU TANGU KUANZISHWA KWA MKOA 2015
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe Happiness Seneda amesema Mkoa wa Songwe ni Mkoa kitinda mimba hapa Nchini ukiwa ni Mkoa wa 26 katika Mikoa yote 26 Tanzania bara na ulianzishwa mwaka 2015 kwa tamko la Mheshimiwa Rais.
Akiongea katika Sherehe za Muungano Mkoani Songwe zilizofanyika Wilayani Mbozi Seneda ameyataja mafanikio ya Mkoa baada ya kuanzisha kwake katika programu mbalimbali za Elimu ambazo baada ya muungano na kwa awamu mbalimbali za Uongozi.
" Mkoa wetu wa Songwe tunayo mafaniko katika Elimu kwa kipindi hiki cha awamu ya sita ya uongozi chini yake Daktari Samia Suluhu Hassani na kwa kweli ameupiga mwingi na anaendeleaje kuupiga mwingi" alisema Seneda
Yafuatayo ni mafanikio sita ya Elimu Mkoa Songwe
- Mkoa ulinza na shule za msingi 393 kwa kuna shule 554. Shule za sekondari toka 86 hadi 154
- Uanzishwaji wa elimu bure ambapo umewezesha kupanda kwa takwimu za wanaohitimu kidato cha nne kuanzia mwaka 2021 wahitimu 8,417 na mpaka 2023 wahitimu 9,457
- Uwekezaji wa fedha kwenye sekta ya elimu katika Mazingira ya kufundisha na kujifungia kwa miaka 5 Mkoa Umepokea jumla ya sh Bilioni 31,444,296,543.56 kwa ajili ya Ujenzi wa miundombinu ya shule za msingi na sekondari.
- Ongezeko la wanafunzi wa sekondari ya kutoka 54,627 hadi 57,424
- fedha za Ujenzi wa miundombinu kwa elimu ya msingi na sekondari chini ya mpango wa elimu bila malipo ni bilioni 26
- Idadi ya shule za msingi zilizosajiliwa za serikali imeongezeka kutoka 393 hadi 480
Kwa ujumla sekta ya elimu kwa miaka 5 ya uwepo wa Mkoa Umepokea jumla ya bilioni 56 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na uendeshaji.
Comments