TANZANIA NA ZAMBIA ZATATUA KERO NNE ZA KIBIASHARA, MAWAZIRI WA VIWANDA KUKUTANA TUNDUMA LEO
Tanzania na Zambia zimefanikiwa kufuta kero nne kati ya keo 15 zilizokuwepo awali ili kirahisisha michakato ya kibiashara na nchi hizo kutegemeana kibiashara.
Hayo yamesemwa Jumatano Aprili 17, 2024 na Katibu Mkuu wa Wizra ya Viwanda na Biashara wa Tanzania, ndugu Hashil Abdallah wakati wa kikao cha pamoja cha makatibu wakuu wa nchi zote mbili katika sekta hiyo.
Akizungumza katika kikao hicho, ndugu Hashil amesema kuwa kikao hicho ni utekelezaji wa maelekezo ya wakuu wa nchi zote mbili Tanzania na Zambia ambao walikutana jijijni Lusaka mwezi Oktoba, 2023 ambapo miongoni mwa makubaliano ni pamoja na mawazili wa pande mbili wanaohusika wakae na watatue changamoto zinazowagusa wafanyabiashara katika nchi hizo.
“Kikao hiki lilikuwa cha makatibu wakuu na kikao cha mawazili kitafanuika kesho (Leo Alhamisi) hapa mpakani Tunduma. Tunatarajia kikao hicho kitakuwa muhimu zaidi katika utatuzi wa kero na changamoto mbalimbali za ufanyaji biashara katika nchi zetu hizi” amesema Katib Mkuu huyo na kuongeza;
“Tuliingia katika majadiliano haya tulikua na changamoto 15 na ndani ya siku tatu hizi tumeweza kutatua kabisa changamoto nne na katika hizo nne mbili zilikuwa upande wa Zambia na mbili zilikuwa Tanzania. Tunatarajia kesho (Leo) kwenye ngazi ya mawaziri changamoto nyingi zaidi zitaweza kuwa zimetatuliwa zaidi” amebeinisha
“Jambo la msingi wenzetu wa Zambia walikuwa wanashindwa ku-proses mizigo kwa haraka pale boda changamoto kubwa walikuwa hawana scanner, tunamshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutoa scana kwaajili yao. Na ilichukua muda mrefu kupokea lakini tunafuraha juzi wameandika barua kuwa wameipokea na wako tayari kwenda kuifunga”
Ameeleza kuwa Zambia kulikuwa na vizuizi vingi kutoka mpakani hadi kufika jijini Lusaka ambapo sasa vimepunguzwa kutoka 33 vilivyokuwepo awali mpaka 11.
“Kwakweli ni hatua kubwa wenzetu wa Zambia wameweza kufanya kuhakikisha ina-facilitate biashara ndani ya nchi zetu. Kubwa lingine sio changamoto ya kibiashara ni maelekezo ya wakuu wetu kuhakikisha tunaanzisha mchakato wakutengeneza boda nyingine kule Kasesya ambayo itaunganisha nchi zetu hizi mbili ni hatua kubwa na kikao hiki kimethibitisha kwamba tayari timu imeshaandaliwa michakato kuanza” amebainisha
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara nchini Zambia, Bi Lilian Bwalya amesema kuwa changamoto zi;lizotauliwa zina maslahi kwa nchi zote mbili.
“Tumetatua baadhi ya changamoto zilizokuwa zinamaslahi kwa nchi zetu zote mbili Tanzania na Zambia kurahisisha ufanyikaji wa biashara ikiwa ni kuongeza wafanyakazi, na kutoa vizuizi vingi njiani ambavyo vilikuwa vinasababisha foleni”
“Katika kero 15 tumeweza kutatua kero nne ambazo mbili zilikuwa upande wa Zambia na mbili upande wa Tanzania. Tumetatua changamoto ya scana ambayo kutokana na mahusiano ya kidiplomasia tumepewa kutoka Tanzania. Tunaamini changamoto zilizobaki mawaziri wetu wakikutana watatatua zaidi kwa maslahi mapana ya nchi zetu ili kurahisisha ufanyikaji wa biashara” amesisistiza
Naibu Mkaguzi Mkuu wa Polisi (Deputy Inspector General of Police) nchini Zambia, Bi. Alita Mbahwe ameishukuru kamati hiyo ya mazungumzo ambayo kwa muda mfupi imeweza kufikia makubaliano bila migongano ya mawazo.
“Watu wengine wanakuwa kama maadui na ni vigumu kufikia muafaka lakini tupo hapa nchi mbili tunacheka na tunafuraha tumefanya kazi nzuri kwakweli na hii ni kitu cha kukiendeleza hata katika mikutano mingine”
Comments