VIONGOZI MKOA WA SONGWE WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYABIASHARA
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Zanzibar, Mhe. Omar Said Shaban ametoa wito kwa viongozi waliopo mkoa wa Songwe kuhakikisha wanatatua changamoto za wafanyabiashara wa mkoa huo ili zisigeuke kuwa kero.
Ametoa wito huo leo Alhamisi Aprili 18, 2024 wakati alipotembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe iliyopo Nselewa, Mbozi.
"Serikali zetu zote mbili zinadhamira ya dhati wananchi wake waweze kufikia malengo yao kwa kutatua changamoto wanazokabiliana nazo ili wajikwamue kiuchumi"
Hii ndio faida ya Muuungano, niwashukuru kwa kuendelea kuijenga Songwe katika taarifa yenu mmeonesha mafanikio na changamoto pia njia za kukabiliana na changamoto hizo" amesema
Ameeleza kuwa Songwe ni mkoa wa kimkakati ambao unanufaika na furasa zinazopatikana katika nchi jirani.
"Tupo mpakani tunapakana na nchi zenye fusa za kibiashara Songwe ni geti kuu la nchi za SADC ikiwa na geti linalopitisha fursa mbalimbali za ajita uwekezaji, uzalishaji pamoja na kilimo" ameeleza
"Mimi kazi kubwa iliyonileta huku ni kwenda kwenye mazungumzo kutatua changamoto za biashara kati ya Tanzania na Zambia. Watanzania na majirani zetu wanamatarajio makubwa sisi viongozi tunawajibu mkubwa wa kuwasaidia"
Comments