SIGARA ZA MAGENDO NI HATARI KWA UCHUMI WA NCHI

 


WADAU wa maendeleo mkoani Songwe wametakiwa kuunganisha nguvu kwa pamoja katika mapambano dhidi ya biashara haramu ya Sigara ili kulinda mapato ya serikali na afya ya umma, ikiwemo kuimarisha amani na usalama wa Taifa.


Rai hiyo, imetolewa Aprili 19, 2024 na Mkuu wa Wilaya ya Ileje, Frida Mgomi, wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku moja ya ya kujadili biashara haramu ya sigara Mkoa wa Songwe iliyoandaliwa na kwa pamoja kati ya Kampuni ya sigara Tanzania (TCC) na ofisi ya Mkuu  ya Mkoa.


Mgomi ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo katika kikao hicho,  amesema kuwa, matokeo hasi yatakayotokea ikiwa biashara haramu ya sigara itaachwa bila uangalizi ni hatari kwa uchumi na usalama wa nchi kwa kuwa biashara haramu ya sigara ndio biashara kubwa haramu ya bidhaa kwa thamani na ya pili baada ya dawa za kulevya kwa mapato yatokanayo na magendo.


"Tunajua kuwa kuwepo kwa sigara za magendo na soko haramu husababisha ukwepaji kodi kwani mapato hayo yanayopotea yangeweza kutumika katika kuboresha utoaji wa huduma za umma kama vile afya, elimu na miundombinu" amefafanua Mgomi.


Ameongeza kuwa utafiti unaonesha kuwa faida itokanayo na biashara haramu ya sigara mara nyingi huishia kwenye mifuko ya mashirika ya kihalifu na hivyo kuchochea shughuli nyingine haramu na kuhatarisha usalama wa nchi.


Aidha, Magomi amesema kuna tishio la kiafya kwa umma linalosababishwa na biashara haramu ya sigara bandia  ambazo hazina viwango vya usalama kwa kuwa mara nyingi zimekuwa na viambata hatari visivyokubalika katika kanuni za afya.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Songwe, Happiness Seneda, ameitaka kampuni y sigara Tanzania kushusha hadi ngazi za chini mipango ya utoaji elimu kwa jamii ili kujenga uelewa juu ya bidhaa bandia na magendo, ikiwemo kushirikisa kamati za usalama za wilaya ili kudhibiti wimmbi la biashara haramu hasa maeneo ya mpakani


Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya sigara Tanzania (TCC), Takahashi Araki, amesema kuwa biashara haramu ya sigara za magendo ni kubwa katika maeneo ta mpakani hali ambayo yanasabaisha serikali kupoteza mapato makubwa na kudhoofisha hali ya ushindani sokoni.


Araki amesema katika kipindi cha mwaka wa 2023 kampuni ya sigara Tanzania iliongeza hali ya uzalishaji wa sigara nchini kwa kuzalisha sigara bilioni 6.5 na kulipa kodi ya serikali kiasi cha shilingi 325.9 bilioni.


Awali akieleza dhumu la warsha hiyo, Mkurugenzi wa uhusiano na mawasiliano wa kampuni ya sigara Tanzania, Patrcia Mhondo, amesema lengo la warsha hiyo ni kutmweka mikakati ya pamoja ya kumaliza tatizo hilo la biashara haramu ya sigara na bidhaa za magendo hususani katika maeneo ya mpakani.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE