WATANO WAKAMATWA MAUAJI NGWALA,SONGWE
Kutokona na uwepo wa matukio ya mauaji katika wilaya ya Songwe mkoani hapa,mkuu wa wilaya ya Songwe Solomon Idunda ameagiza kila Kijiji kianzishe vikundi vya ulinzi shirikishi (Sungusungu) ili kulinda na kupunguza uharifu.
Itunda ameyasema hayo 28 Mei,2024 waka ti wa ziara ya mkuu wa mkoa a kijiji na kata ya Ngwala.
Amesema kumekuwa na baadhi ya Viongozi wa serikali ya vijijini wanaendekeza rushwa wakiwaingiza kiholela wageni jamii wafugaji na kusababisha migogoro.
Siku za hivi karibuni kuna mauaji yalitokea na hii imesababiahwa na uwepo wa wageni wengi wanaoingia kinyemela Ngwala na kwamba hadi sasa Wananchi watano wamekamatwa wanaendelea kuhojiwa.
Hatua hiyo ya mkuu wa wilaya imekuja baada ya wakazi wa kijiji hicho wa kiongozwa na Samuel Michael kueleza hali ya mauaji ikiwemo migogoro ya ardhi .
Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo amesema ni marufuku Viongozi wa vijiji kupokea wafugaji pasipo kibali kutoka ofisi ya mkuu wa wilay a na pia amemuagiza Mk uu huyo wa wilaya kufanya sensa ya mifugo na inayozidi iondolewe.
Comments