CHONGOLO AWATAKA WANANCHI KUTUMIA TAA ZA MJI WA MKWAJUNI KUKUZA FURSA ZA MJI
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo amewataka Wakazi wa Mkwajuni Songwe kuendana na kasi ya maendeleo yanayoletwa na serikali ambapo amewataka kutumia fursa ya taa zilizofungwa barabara za miji ya Mkwajuni Wilayani humo.
Akiongea mapema leo asubuhi 27 mei,2024 amesema amefurahishwa na taa zilizofungwa na uwekaji wa Barabara za lami zilizotokana na fedha za mfuko wa Jimbo ambapo Chongolo amesema kuwa taa hizo nyakati za usiku Wananchi watumie kufanya biashara ili kujiongezea kipato.
"Hizi taa zisiwe kama urembo tu tumieni taa hizi kufanya biashara usiku ili hata wageni wakija usiku hapa Mkwajuni angalau wapate hata chakula usiku na nyie Halmashauri mkiona watu wanakesha kufanya biashara basi nanyi watu wa mapato mkeshe hapa ili wote mtimize wajibu kwa pamoja.
Katika hatua nyingine Chongolo amempongeza Mbunge wa Wilaya ya Songwe Philipo Mulugo kwa uamuzi wake wa kuwashauri Madiwani na Halmashauri kwa ujumla fedha za Jimbo Milioni 500 zielekezwe katika Ujenzi wa barabara za Mji wa Mkwajuni badala ya kuzitawanya maeneo mbalimbali lakini waliona waziweke sehemu moja hivyo ili kuutupa hadhi mji.
Chongolo ameanza ziara Wilayani Songwe ya siku tatu yenye lengo la kujitambulisha na kukagua Miradi ya
Comments