MIAKA 30 JELA KWA WIZI WA SIMU

Mahakama ya Hakimu mkazi mfawidhi mkoa wa Lindi imemuhukumu Naimu Ally M'baruku @ Soggy, mwenye miaka 20, mkazi wa mtaa wa Ndoro manispaa ya Lindi kwenda Jela kifungo cha miaka 30 kwa kosa la kunyang'anya simu aina ya TECNO SPARK 8 kwa kutumia silaha (Panga).


Aidha Mahakama hiyo imewahukumu Zuberi Saidi Mnape mwenye miaka 47, mkazi wa Kiangala, Liwale - Lindi, Jemedari Hemedi Mpulumila mwenye miaka 67, mkazi wa Mbagala - Dar es salaam na Mohamedi Juma Mbacho mwenye miaka 49, mkazi wa Nachingwea - Lindi kwenda Jela kifungo cha miaka Ishirini kila mmoja au kulipa faini ya shilingi milioni mia sita tisini na sita (Tsh.696,000,000/=) kwa makosa ya Kupatikana na Nyara za Serikali (Meno na Pua ya Tembo), Kumiliki Silaha (Bunduki) kinyume na sheria, Kumiliki milipuko/vilipushi (Risasi) kinyume na sheria na Kuua wanyamapori (Tembo) kinyume na sheria.

Katika hatua nyingine Mahakama ya wilaya ya Kilwa imemuhukumu Kamugisha Filbert Lugemalila mwenye miaka 47 na Jamilu Swaibu Kichwabuti mwenye miaka 25 wote wakazi wa Dar es salaam kwenda jela kifungo cha miaka mitano kika mmoja kwa kosa la Wizi (Vifaa mbalimbali kwa ajili ya kazi ya kuchukulia Video).

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UDUMAVU BADO TISHIO -DUGANGE

SONGWE JOGGING WARUDI NA MEDANI ZAIDI YA KUMI NA TANO TULIA MARATHON

MOMBA HAWANA JAMBO DOGO: ROUTE VIONGOZI NA WANANCHI WAKUTANA PAMOJA ROUTER MATCH YANOGA