MKUU WA MAGEREZA TANZANIA AMPA MTAJI MFUNGWA ALIEMALIZA KIFUNGO CHAKE
Kamishna jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP)Mzee Ramadhani Nyamka Mei 23,2024 amemtembelea Ndugu Thimotheo Silas ambaye alikua mfungwa aliye maliza kifungo chake katika Gereza Kuu Butimba mwaka 2019.
Aidha Kamishna Jenerali amemkabidhi kiasi cha fedha Shilingi Laki Tano kwaajili ya kuongezea mtaji wa uendelezaji wa Bustani ya mbogamboga eneo la Butimba Jijini Mwanza.
Cgp nyamka amesema kuwa msaada huo aliompa ni chachu kwa wafungwa wengine watakaomaliza vifungo vyao na kurudi makwao na kufuata yale yote waliyo fundishwa magerezani katika dhana nzima ya urekebu.
Wakati huohuo Kamishna Jenerali amemuagiza Mkuu wa Magereza Mkoa Mwanza, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza (SACP) Justine Kaziulaya kumtafutia mfungwa huyo aliyemaliza kifungo chake eneo la ekari tano kwaajili ya kufanyia shughuliza kilimo ambapo litamsaidia kumuongezea kipato kwakua ameonyesha kurekebu mara baada ya kutoka gerezani.
Hata hivyo CGP Nyamka ametoa rai kwa wananchi kuwa mfungwa anapotoka gerezani anakuwa tayari amerekebika hivyo jamii isimnyanyapae na kumtenga badala yake imshirikishe katika masuala ya kijamii ili ajione ni mwana jamii na asiweze kurudi tena gerezani.
Amesema jeshi la magereza jukumu lake kubwa la msingi ni kuhakikisha linatoa elimu ya urekebu kwa wafungwa wanao ingia magerezani ili wakitoka wawe watu wema kwenye jamii
Comments