POLISI KATA NANGULUKULU ILEJE AWAHAKIKISHIA USALAMA WANANCHI WAKE

Wananchi wa Kata ya Ngulugulu iliyopo wilayani Ileje wametakiwa kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu katika maeneo yao kwani huduma ya Polisi imeletwa karibu yao.


Kauli hiyo imetolewa Mei 23, 2024 na Polisi Kata ya Ngulugulu Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Neema Minja wakati akizungumza na wananchi hao kwa lengo la kuwajengea uelewa kuhusu umuhimu wa ulinzi jirani katika maeneo yao ili kuzuia uhalifu.

“Huduma ya Polisi kwa sasa inapatikana katika ngazi ya chini kabisa kuanzia kata kwa hiyo ondoeni wasiwasi wa kiusalama kuweni huru katika shughuli zenu za kila siku bila kuwa na shaka kwani mimi nimeletwa kwa ajili yenu, mnachotakiwa ni kunipa ushirikiano wa kutoa taarifa za uhalifu na vitendo vya ukatili wa kijinsia ili kata yetu iendelee kuwa salama” alisema Mkaguzi Minja.


Aidha, Mkaguzi Minja aliwasihi wananchi hao kuendelea kuimarisha ulinzi hasa ukizingatia jiografia ya Kata hiyo inapakana na nchi jirani ya Malawi hivyo kufanya kuwa na muingiliano wa wa watu ambao hawafuati utaratibu wa kiserikali na kusababisha migogoro hasa ya ardhi pindi muwaonapo watu hao toeni taarifa kwa viongozi ili waweze kushughulikiwa haraka ikiwemo kufikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE