RAIS WA IRAN AMEPOTEA NA HELIKOPTA ILIOMBEBA

 


Helikopta iliyombeba Rais wa Iran, Ebrahim Raisi na wasaidizi wake imepata ajali katika eneo la magharibi mwa nchi hiyo, huku chanzo kikitajwa kuwa ni hali mbaya ya hewa katika eneo hilo.


Waziri wa Mambo ya Ndani wa Iran, Ahmad Vahidi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo lakini hajaeleza zaidi.

Amesema itachukua muda kupata eneo helikopta hiyo ilipopata ajali kutokana na hali hiyo mbaya ya hewa ikiwa ni pamoja na ukungu mwingi, na kwamba timu mbalimbali za uokoaji kwa sasa zinaitafuta helikopta hiyo.

Rais wa Azerbaijan, Ilham Aliyev ameeleza kushtushwa na ajali ya helikopta hiyo iliyombeba Rais Ebrahim Raisi.

Kabla ya ajali hiyo Aliyev alikuwa na Rais huyo wa Iran katika ufunguzi wa mabwawa mawili karibu na mpaka wa Iran na Azerbaijan.

Amesema Azerbaijan iko tayari kutoa msaada wowote unaohitajika ili kuweza kubaini ilipo helikopta hiyo.

Rais Raisi alikuwa akisafiri na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran katika msafara wa helikopta tatu ambapo helikopta mbili kati ya hizo zimeripotiwa kutua salama.

Raisi alichaguliwa kuwa Rais wa Iran mwaka 2021

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UDUMAVU BADO TISHIO -DUGANGE

SONGWE JOGGING WARUDI NA MEDANI ZAIDI YA KUMI NA TANO TULIA MARATHON

MOMBA HAWANA JAMBO DOGO: ROUTE VIONGOZI NA WANANCHI WAKUTANA PAMOJA ROUTER MATCH YANOGA