RC -CHONGOLO ATANGAZA KIBANO KULINDA USALAMA WA NCHI KWA WATAKAOJIINGIZA KUVUSHA RAI WA KIGENI KINYEMELA
Amesema zipo nchi nyingi za afrika hali ya usalama sio mzuri,mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yapo ,hivyo wanasongwe wanakila sababu ya kulinda usalama uliopo nchini kwa kutowakaribisha wageni kuingia nchini kinyemela kwa ni hatari.
‘’Raia hao wa kigeni mnapowakaribisha nchini hamjui wamebeba nini wanaweza kuleta hatari kubwa na madhara kwa nchi,hivyo kila mmoja awe mlinzi wa mwenzie,umuonapo mtu usiyemfahamu toeni taarifa kwenye oungozi uliopo karipo nanyi ikiwemo polisi kata.’’amesema Chongolo.
Amesema wilaya ya Momba imepakana na nchi za Congo na Zambia,inawezekana raia wa nchi za mbali wakapitia nchi hizo kuja Tanzania ili wevuke kinyemela kwenda nchi zingine,hivyo lazima taarifa zitolewe kwa mtu ama watu watakaowaona raia wa kigeni maeneo yao ili wahusika wa biashara hiyo wakama twe na kuchukuliwa hatua.
“Hapa nipo na jeshi la polisi,Magereza,uhamiaji,usalama wa Taifa,Mshauri wa mgambo,na wakuu wa taasisi mbalimbali,nalisema hili na wao wanasikia,atakayekamatwa atashitakiwa na kufikishwa maha kamani,hivyo acheni kujihusisha na kazi hiyo’’,amesema.
Nae kamanda wa Polisi mkoani Songwe,Augostino Senga amesema wamejipanga kuhakikisha wana simamia na kulina amani ya nchi iliyopo,atakayeenda kinyume au kijiingiza na uharifu na hata kusa firisha raia wa kigeni atakamatwa na kupekekwa mahakamani.

Maoni