RC SONGWE AITAKA JAMII KUSOMESHA WATOTO WA WA KIKE KWA KUWA NI MSAADA MKUBWA



Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewashauri wazazi na walezi katika Wilaya ya Songwe kuhakikisha wanawasomesha watoto wa kike kama wanavyowasomesha wa kiume kwani watoto wa kike wanapoolewa ndio wanajali wazazi wao kuliko wa kiume.

Chongolo ambaye ashawahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CMM) ametoa ushauri huo wakati akiongea na wananchi wa mji wa Mkwajuni  ikiwa ni siku yake ya kwanza ya kuanza ziara ya siku tatu Wilayani Songwe.

Chongolo ambaye ameanza ziara kwa kukagua mradi wa uwekaji taa katika barabara zilizo chini ya TARURA katika mji wa Mkwajuni, amesema kuwa ili kupunguza hali ya mdondoko wa wanafunzi katika Wilaya hiyo pamoja na mkoa wa Songwe, lazima wazazi na walezi kuhakikisha watoto wa kike wote wanapata elimu kama wa kiume.

"Kuna suala la mdondoko wa wanafunzi kwenye shule zetu hasa watoto wa kike. Kuna mambo ambayo yanasababisha mdondoko huo kama mimba, kuacha shule watoto ili waende kuwa dada wa kazi, uchimbaji, kilimo na ufugaji. Wazazi hakikisheni watoto wa kike wanapata elimu hawa ndio wanawakumbuka kuliko sisi wanaume" amesisitiza.



Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE