RC SONGWE ATOA SIKU 14 KWA TANESCO KUPELEKA UMEME NAMBALA



MKUU wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo atoa siku 14 kwa meneja wa Shirika la Umeme tanesco kuweka umeme kijiji cha Nambala kilichopo Mbozi Mkoani Songwe.

Chongolo ameyasema hayo leo Mei 24/2024 kwenye mkutano wa baraza la biashara mkoa uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano mkoa.

Ameyasema hayo baada ya mwananchi Rosmery Mwakingili mkazi wa Nambala kutoa kero hiyo mbele ya mkutano akieleza kukerwa na ukosefu waumeme. 

Amesema eneo la Nambala ndiko zilipo ofisi za mkoa cha ajabu eneo la ifisi na nyumba za Serikali umeme upo lakini eneo la makazi ya watu hakuna umeme. 

Baada ya maelezo hayo mkuu wa mkoa alimuonua Meneja wa Tanesco mkoa kutoa majibu. 

Akitoa majibu hayo kaim meneja wa shirika la umeme (Tanesco) mkoani Songwe Mhandisi Dismas Temba amekuri kuwepo kwa changamoto hiyo huku akiahidi kuitatua. 

Amesema wilaya ya Mbozi ina vitongoji 666 kati ya hivyo vitongoji 284 havina umeme na 190 vipo kwenye utekelezaji. 

“Mh.mkuu wa mkoa hapa Songwe tunatumia chanzo cha Mwakibete kilichopo Mbeya kupata umeme  ambapo ni kilometa 70 hivyo tuna mipango ya kuanza kujitegemea “ amesema.

Naye mkuu wawilaya ya Momba Kennan Kihongosi amesema kwa kiliona hilo Serikali kmetoa Bilioni 370 kujenga mradi utakao kuwana wats laki 4 wilayani Momba na utakuwa na uwezo wa kuwasha umeme mkoa mzima. 

Akitoa msisirizo huo  mkuu wa mkoa Chongolo amesema mradi huo usimamiwe na wakandarasi waongeze Jitihada zaidi kuhakikisha unakamilika kwa wakati ili wananchi waanze kutumia umeme bila vikwazo. 

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE