TANI 500,000 ZA MAHINDI MEUPE KUUZWA JAMHURI YA DEMOKRASIA YA CONGO (DRC)

Serikali imeendelea kuhakikisha upatikanaji wa masoko ya uhakika ya mazao ili wakulima wazidi kunufaika na bei nzuri ya mazao ma uhakika wa usalama wa chakula nchini na katika nchi za jirani.


Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa mauziano ya mahindi meupe baina ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi Chakula (NFRA) na Kampuni ya Quincy kutoka Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) tarehe 21 Mei 2024, jijini Dodoma.


Mkataba huo umesainiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa NFRA, Dkt. Andrew Komba pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Quincy, Bw. Yuma Jesse huku ukishuhudiwa na Gavana wa Jimbo la Katanga, Bw Jacques Kyabula Katwe pamoja na Katibu Mkuu Mweli.

Mkataba huo unahusisha awamu mbili za mauziano ya mahindi ambapo kwa awamu ya kwanza nchi ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC) itakabidhiwa tani 200,000 za mahindi meupe huku tani 300,000 za mahindi hayo zikitarajiwa kukabidhiwa katika awamu ya pili ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa chakula uliosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.

Dkt. Andrew Komba amewahakikishia wakulima upatikanaji wa masoko ya uhakika kwani NFRA itaendelea kununua mazao ya wakulima na kuyauza katika masoko mbalimbali huku ikihifadhi ili kuhakikisha usalama wa chakula nchini unakuwepo.

Dkt. Komba amefafanua kuwa hadi sasa jumla ya tani 500, 000 za mazao zimehifadhiwa huku mazungumzo na nchi nyingne ikiwemo Zambia yakiendelea kwa ajili ya upatikanaji wa soko la mazao katika nchi hiyo.

Naye Gavana wa Jimbo la Katanga Bw. Jacques Kyabula Katwe ameishukuru Serikali kwa ushirikiano ilioyouonesha ambao umezidi kuboresha uhusiano mwema baina ya Tanzania na Congo-DRC, na kuahidi kuendeleza ushirikiano huo kwa maendeleo ya pande zote mbili.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UDUMAVU BADO TISHIO -DUGANGE

SONGWE JOGGING WARUDI NA MEDANI ZAIDI YA KUMI NA TANO TULIA MARATHON

MOMBA HAWANA JAMBO DOGO: ROUTE VIONGOZI NA WANANCHI WAKUTANA PAMOJA ROUTER MATCH YANOGA