UKATILI WA KUTISHA RC NA RPC SONGWE WASHANGAZWA MTOTO WA MIAKA 2 KUBAKWA HADI KUFA KWENYE SHAMBA LA MAHINDI
Na Ibrahim Yassin,Songwe
MKUU wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo,kwa kushirikiana na kamati ya usalama ya mkoa,ametangaza vita kwa watu wan aoendekeza vitendo vya ukatili kwa Watoto ikiwa ni Pamoja na mauaji yanayotokana na wivu wa kimapenzi na Imani za kishirikina wanazoshauriwa na baadhi ya waganga wa kienyeji.
Chongolo ameyasema hayo,leo Mei/16/2024 alipokuwa akizungumza na wananchi wilayani Momba katika ziara yake ya kuji tambulisha baada a Rais Dkt,Samia kumteua kuwa mkuu wa mkoa iliyoenda sambamba na kukagua miradi ya maendeleo.
Amesema kitendo cha baadhi ya wananchi wanaoshindwa kupanga mikakati ya kubuni njia sahihi za kutafuta fedha wana enda kwa waganga wa kienyeji ambao wanawaeleza kuwa ili wapate mahali abake mtoto wake kitu ambacho ni uongo wa hali ya juu.
''hivi hao wanganga wanaotoa maelezo hayo kwa wateja zao,wenyewe hali zao zipoje?,ninyi wananchi achene kudanga nywa,eti unaambiwa ili upate mavuno mengi au dhahabu nyingi basi umbake mtoto tena wa kumzaa na wewe unakubali alafu matokeo yake unaendelea kuwa masikini,acheni Imani hiyo ni potofu''amesema Chongolo.
Hata hivyo Chongolo amesema yeye na kamati yake ya usalama,wamejipanga vizuri kuhakikisha wanashughurika na wale wote wanaoendesha vitendo hivyo,huku akimuinua mkuu wa polisi mkoa kueleza yaliyotokea siku mbili zilizopita.
Kamanda wa polisi mkoani Songwe Augostino Senga,amewatahadharisha wananchi kuacha kujiingiza kwenye vitendo vya kikatili,na kusema jeshi lake limejipanga kuhakikisha linawatia hatiani watakaobainika kuendesha vitendo hivyo vya ukatili hasa wa kingono.
Amesema siku za hivi karibuni,mtoto wa miaka 2 alibakwa na kutelekezwa kwenye shamba la mahindi wilayani Songwe na baada ya jeshi kupata taraifa walienda eneo hilo na kukuta mtoto amefariki,baada ya maumivu na njaa.
Amesema mbali na tukio hilo pia kuna baba anatuhumiwa kumbaka mtoto wake wa kumzaa kwa Imani eti atapata mafanikio ya Maisha na kwamba huo ni ukatili mkubwa na ni aibu mbele ya jamii.
''Mimi ninamwezi mmoja na nusu toka niletwe mkoa huu wa Songwe,nimekuta baadhi ya matukio ya aina hii yameto kea,hatawaacha salama,wahusika wote tutawakamata,nawasihi ndugu zangu waacheni Watoto wasome,msijiingize kwenye matukio hayo''amesema Kamanda Senga.
Aidha Kamanda Senga amesema hivi majuzi tu,kuna mtu jina ambaye ni mkazi wa halmashauri ya Tunduma amehukumiwa kutumikia kifungo cha miaka Zaidi ya 30 jela baada ya kukutwa na hatia ya kubaka mtoto,na kwamba watakaoendekeza tabia hiyo watashughulikiwa.

Maoni