VOCHA ZA MITANDAO YA SIMU ZADAIWA KUPANDISHA BEI KIHOLELA MBOZI
Wafanyabiashara katika Mji wa Mlowo,Mbozi wamedaiwa kupandisha vocha za mitandao ya simu toka bei halisi na kuongeza kiwango kati ya shilingi 100 hadi 200 kutokana na eneo hali ilioibuka malalamiko kwa watumiaji wa mitandao ya simu.
Wakiongea malalamiko yao mbele ya mwandishi wetu wamedai imekuwa ni kawaida ya wafanyabiashara kupandisha vocha hasa kipindi hiki cha kuelekea katika bajeti
"Tunaomba serikali iwachukulie hatua na kuwatia hatiani baadhi ya wafanyabiashara ambao sio waamini mfano vocha ya 500 tunanunua 600 na vocha ya 1000 tunanunua 1200 sasa huku ni kutuumiza jamani" alisema John Milango mkazi wa forest
Akiongea mmoja wa wafanyabiashara wa vocha ambae aliomba jina lake lihifadhiwe alidao nao wamekumbana na ongezeko la bei toka kwa wafanyabiashara wa jumla wa vocha wamewapandishia bei ya vocha hivyo imepekea nao kupandisha.

Comments