WAFANYABIASHARA SONGWE WALALAMIKA FOLENI YA KUSIMAMISHIA MAGARI SENJELE NA NANYALA WILAYANI MBOZI


Mwenyekiti wa chemba ya wafanyabiashara Mkoa wa Songwe TCCIA Charles Chenza ameomba Vituo vya kusimamishia magari vya Senjele na Nanyala vilivyopo Wilayani Mbozi viondolewe kwani vimekuwa ni kero kwa Wafanyabiashara na Wananchi kwa ujumla kutokana na kukaa muda mrefu wakisubiri  foleni ya kupishana magari makubwa na madogo 


Akiongea katika kikao cha  baraza la Biashara la Mkoa wa  Songwe lililofanyika katika ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Songwe leo 24 Mei 2024 Chenza amedai kuwa kumekuwepo na usumbufu usiokuwa na ulazima wowote wa watu kukaa muda mrefu katika foleni hiyo hivyo amemuomba Mkuu wa Mkoa Daniel Chongolo kama Mwenyekiti wa Usalama Mkoa wa Songwe kuwasaidia kero hiyo.

Akijibu kwa niaba ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe SACP Augustino Senga afisa mnadhimu wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamanda ACP Gallus Hyera amesema wao kama polisi kwa kuwa kituo vituo hivyo vinalalamikiwa watakwenda kujadiliana ikiwa ni pamoja na kupunguza muda wa magari kukaa katika foleni hiyo.


Naye Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo amesema kama ofisi yake wanalipokea na watakwenda kulijadili kwa kina na watapata majibu ya kina aidha wavifute vituo hivyo ama laa.

" Niwaombe hili tunalipokea na tunakwenda kujadilia hili ili tujue sababu zipi zilisababisha vituo hivyo kuwepo na namna bora ya kuviboresha ili kuondoka kero hii ya kukaa muda mrefu" alisema Chongolo

Kikao cha baraza la wafanyabiashara ni utaratibu wa kuwakutana wafanyabisha na wadau mbalimbali ili kujadiliana changamoto na utekelezaji wa maadhimio mbalimbali ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Mheshimiwa Rais.

Comments

Popular posts from this blog

MAKONDA AWACHANA MAKAVU KATIBU CCM NA UVCCM SONGWE