"WAFANYABIASHARA TUMIENI FURSA YA STENDI YA MLOWO KUJIONGEZEA KIPATO" RC CHONGOLO


 Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo amekagua zoezi la maboresho ya miundombinu na  uunganishwaji wa vyumba vya biashara na pia kuagiza  wajasiriamali wote kuanza biashara zao ndani ya stendi ya mabasi Mlowo


Hatua hiyo imekuja baada ya vibanda hivyo vilivyojengwa hapo awali kuwa ni vidogo ambapo Mhe. Chongolo aliagiza vibanda hivyo kurekebishwa kwa kuunganisha vyumba viwili kuwa kimoja.

Mkuu wa Mkoa huyo ametoa wito kwa wafanyabiashara kutumia fursa hiyo kuuza biashara zao kuongeza kipato


‘’Kituo chetu hiki kiwe senta ya mauzo au biashara cha mkoa kwahiyo wananchi watumie hii fursa kama hatupo tayari watakuja walio tayari’’ amesema 


Ameahidi kuwa atarudi tena katika stendi hiyo ili kuona mchakato unaendeleaje na kuangalia mpangilio wa mabasi na wajasiliamali unaendaje.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

UDUMAVU BADO TISHIO -DUGANGE

SONGWE JOGGING WARUDI NA MEDANI ZAIDI YA KUMI NA TANO TULIA MARATHON

MOMBA HAWANA JAMBO DOGO: ROUTE VIONGOZI NA WANANCHI WAKUTANA PAMOJA ROUTER MATCH YANOGA