WATOTO ZAIDI YA 194 WAPEWA MIMBA NDANI YA MWEZI MMOJA MOMBA
Zaidi ya watoto 190 Wilayani Momba wamepewa ujazito na kupelekea kuacha masomo
Kauli hiyo imetolewa leo Mei /2024 na mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo alipokuwa aki zungumza na wananchi Kijiji cha Naming"ong"o Wilayani Momba.
Amesema kitendo cha wanaume kuwapa ujau zito wanafunzi hakiku baliki,hivyo ame liagiza jeshi la Polisi kuhaki kisha linawaka mata watuhumiwa wote na kufikishwa Mbele ya sheria.
"Wakati mkoa wa Kilimanjaro wana watoto 2 pekee waliopewa mimba hapa Momba mwezi uliopita tu watoto zaidi ya 190 wamepewa mimba" amesema Cho ngolo.
Hata hivyo Chongolo amewaagiza Viongozi wa vijiji na Kata kuhakik isha watoto wanakuwa salama na kutoa taarifa kwa mkuu wa Wilaya kunusuru sakata hilo.

Maoni