WANAKIJIJI MOMBA WACHANGISHANA MIL,18 KUJENGA SHULE KUHEPUSHA WATOTO KUTEMBEA KILOMETA 10 KWENYE SHULE MAMA
Na Ibrahim Yassin,Songwe
Wananchi wa vitongoji vilivyopo kata ya Ikana wilayani Momba mkoani Songwe wamechangishana fedha Milioni 18 kuanzisha shule ya sekondari Ikana kuokoa adha kwa Watoto wao waliokuwa wakitembea umbali wa kilometa 10 kwenda kwenye shule mama ya Chikandamulilo hali iliyofifisha ufauru kwa Watoto.
Akizungumza leo Mei 16/2024 mwenyekiti wa Kijiji cha Ikana Bahati Sikapize amesema baada ya wanafunzi ambao ni Watoto zao kuona wakiteseka kwa muda mrefu wakitembea kilometa 10 kwenda shule ya Chikandamulilo,waliitisha mikutano ya hadhara kuelezana namna ya kujenga shule eneo hilo.
Amesema baada ya kuelezana changamoto hiyo,wananchi wakaridhia kuchangashana fedha na kupatikana Milioni 18 na kuanzisha ujenzi wa shule mpya ya Ikana huku wakitoa maombi serikalini kuongezewa nguvu ya fedha ili malengo yao yatimia na yakatimia.
Kaimu afisa elimu sekondari wilayani humo,Mwl,Hamis Nywange amesema baada ya wananchi kuanzisha mchakato huo,ujenzi ulianza mwaka 2021/2022 na kukamilika 2023 ambapo serikali ilitoa Tsh,Milioni 470 kuunga jitihada za wananchi kukamilisha ujenzi wa shule hiyo.
Amesema mwaka huu wa 2024 wanafunzi wa kidato cha kwanza wameanza kusoma na wananchi tayari wameanza kupata nafuu kuoana Watoto wao wakiondokana na kadhia hiyo ya kutembea umbali wa kilometa 10 kwenda kwenye shule mama ya Chikandamulilo.
Amesema hali hiyo ilififissha kasi ya Watoto kuipenda shule na wengi wao hawakuwa na hamu ya kusoma,lakini kwa sasa baada ya ujenzi wa shule hiyo mpya yenye miundombinu yote anauhakika Watoto wengi wataongeza ufauru kutokana na shule hiyo kusogezwa karibu na makazi yao.
Mkuu wa mkoa wa Songwe Daniel Chongolo, amesema anakila sababu ya kuwapongeza wananchi kwa kuona umuhimu wa elimu kuanzisha ujenzi na kusema Rais Dkt,Samia Suruhu hakusita kutoa kiasi hicho cha fedha cha Milioni 470 kuunga jitihada za wananchi kuikamilisha shule hiyo.
''Shule imejengwa,mmejitolea na serikali imewaunga mkono,hakikisheni wanafunzi wanapata ufauru mzuri,pia wazazi na walezi hakikisheni mnafuatilia mienendo ya Watoto wenu mkishirikiana na walimu,na wale wemye tabia ya kuwanyemelewa wanafunzi achene mara moja kwani mkono wa sheria hauta waacha salama''amesema Chongolo.


Maoni